Skip to main content

AFISA MAENDELEO ASIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANANCHI KWA AJILI YA KUTAFUTA SULUHISHO

Submitted by admin on 25 February 2025

Katika jitihada za kuboresha ustawi wa jamii na maendeleo ya wananchi, Afisa Maendeleo aliendelea kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi ili kutafuta njia bora za kuzitatua.  
Image

Wakati wa mkutano huu, wananchi walipata fursa ya kueleza matatizo yao, huku Afisa Maendeleo akisikiliza kwa makini na kutoa ushauri wa hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuleta suluhisho la kudumu. Lengo kuu la kikao hiki lilikuwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata msaada unaostahili na kuimarisha maendeleo katika jamii.  
Image

Hatua hii ni sehemu ya jitihada za serikali za kusogeza huduma kwa wananchi na kuhakikisha kwamba changamoto zao zinashughulikiwa kwa wakati.

#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya