Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo wamekuwa wakifika kwenye dawati hilo wakiwa na changamoto za kisheria, ikiwemo masuala ya mirathi, ndoa, migogoro ya ardhi, na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia. Afisa huyo amekuwa akiwapokea kwa makini na kusikiliza hoja zao kwa lengo la kuwapa msaada stahiki kwa kufuata taratibu za kisheria na kuwahimiza kufikia suluhisho la amani.
Akizungumza, Afisa huyo alisema, "Lengo la dawati hili ni kuwahudumia wananchi kwa haki na kuhakikisha wanapata suluhisho la kisheria bila upendeleo. Tunazingatia usawa na haki katika kila hatua."
Wananchi waliopata huduma katika dawati hilo wameelezea kuridhishwa kwao na jinsi wanavyopokelewa na kusaidiwa. "Huduma ni nzuri, tunashukuru kwa msaada tunaopewa. Migogoro mingi tunayoleta hapa inashughulikiwa kwa umakini," alisema mmoja wa wananchi aliyefika kwenye dawati hilo.
Dawati la Msaada wa Kisheria Wilaya ya Namtumbo limeendelea kuwa tegemeo kwa wananchi, likihamasisha utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani na kuimarisha mshikamano katika jamii. Afisa huyo pia aliwataka wananchi kujitokeza zaidi na kutumia huduma hizo bila hofu, akisisitiza kuwa msaada wa kisheria ni haki ya kila mmoja.
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango@biteko
@katibanasheria_@prof
.kabudipjam@victoria
.mwanziva @tanganyikalawsociety @boniface_a_k_mwabukusi