JAMII imetakiwa kuandika wosia wa mali zao ili kuepusha migogoro ya mgawanyo wa mali hizo baada ya kifo cha mhusika kutokea. Ofisa kutoka Ofisi ya Wakala wa usajili ufilisi na udhamini (RITA) ,Mohamed Changula alitoa ushauri huo kwenye mkutano wa hadahara Kijiji cha Ipande halmashauri ya wilaya ya Itigi Mkoani hapa mwisho wa wiki walipofika kutoa elimu ya msaada wa kisheria kupitia kampeni ya mama Samia.
Changula alisema jamii inatakiwa kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya mgawanyo wa mali baada ya kifo kutokea.
“Kuandika wosia sio kujichuria kifo kama jamii inavyoamini bali ni ustarabu wa kuandaa mgawanyo wa mali zako ili kuondoa mgogoro pale kifo kitakapokuchukua”alisema.
Alitaja aina mbili za kuandika wosia kuwa ni kwa njia ya maandishi au na mdomo na wosia huo na inatakiwa kuwa ma mashahidi unatakiwa kubaki kuwa siri ili kuepusha mgogoro kwa warithi walioandikiwa.
Alisema wosia huo lazima uthibitishwe na mwanasheria ili kumsaidia mhusika kuzingatia masharti ya kukamilisha mkataba hu ambao mhusika anaweza kuomba uhifadhiwe ofis za RITA kwa usalama na ikitokea mabadiliko ya mashahidi anaweza kubadilisha.
Changula alisema wosia unaanza kufanyakazi pale mhusika anapofariki na mashahidi watawasiliana na ofisi kuwajulisha ili maandishi hayo yafikishwe kwenye kikao cha familia.
Aliongeza kuwa waosia wa tamko (mdomo) lazima ushuhudiwe na watu wanne kati ya hao wawili watakuwa ni ndugu waka karibu na wawili wanaweza kutoka nje ya wanafamilia.
Aidha alisema wanaojitoa kwenye waosia ni kundi watakaofanyajaribio la kutaka kumuua mzazi na wale ambao hawatamhudumia mzazi alipokuwa mgonjwa.
Kuhusu taratibu za usimamizi wa mirathi wanafamilia wanatakiwa kukaa kikao cha watu wasiopungua nane kati ya hao lazima wanne wawe na kitambulisho cha taifa.
Kiongozi wa kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia kwa halmashauri ya wilaya ya Itigi ,Malongo Jackson alisema lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu ya msaada wa kisheria pamoja na kutatua kero za wananchi.
Jackson alisema kampeni hiyo Kimkoa ilizinduliwa januari 10 mwaka huu na wamegawanyika kila wilaya kuwasikiliza wananchi kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara na mtu moja moja.
Alisema matatizo mengi ya wananchi wanayokutana nayo kwenye kampeni hiyo ni migogoro ya ardhi,ndoa na unyanyasaji wa kijinsia pia kampeni hiyo inawataalamu wa kisheria kutoka taaisisi mbalimbali na maofisa ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii na maofisa kutoka madawati ya kijinsi la jeshi la Polisi.
- Log in to post comments