Skip to main content

ARUSHA KUMANOGA!

Submitted by admin on 29 March 2025

Wananchi wa Jiji la Arusha wamejitokeza kwa wingi kufuatia uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria, hatua ambayo inalenga kuwapa fursa ya kupata huduma muhimu za kisheria bila malipo kabisa.

Kampeni hiyo, inayotekelezwa na mashirika mbalimbali ya kisheria kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu, inalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao za kisheria, kuwasaidia katika masuala ya kisheria, na kuwahamasisha kufuatilia haki zao kupitia taratibu za kisheria.

Image

Wananchi waliokuwepo wakati wa uzinduzi huo walielezea shukrani zao kwa kuanzishwa kwa huduma hiyo, wakitaja changamoto za upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa gharama nafuu kama kikwazo kikubwa kwa watu wa kipato cha chini.

Image

Kampeni hiyo inatarajiwa kuendelea kwa muda wa wiki kadhaa, ikiwa na malengo ya kufikia maeneo mengi ya Jiji la Arusha ili kuhakikisha kila mtu anapata nafasi ya kunufaika na huduma hizi muhimu za kisheria.

Image

Aidha, waandaaji wa kampeni hiyo wametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi na kutumia fursa hii ili kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mmoja. @samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa

@hakingowinews @katibanasheria_ #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya