Skip to main content

ASIA SADICK APATA MSAADA WA KISHERIA KUTOKA MSLAC BAADA YA MTOTO WAKE KULAWITIWA

Submitted by admin on 26 June 2024

atika tukio la kuhuzunisha, Asia Sadick, mama mmoja mwenyeji wa eneo la Gongolamboto Majoe, amepata msaada wa kisheria kutoka Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mamama samia (MSLAC) baada ya mtoto wake, Aisha, kudhulumiwa kingono na jirani yao. 

Asia, ambaye alikuwa amepoteza matumaini ya kupata haki, aligeukia MSLAC kwa usaidizi baada ya tukio hilo ambalo lilipelekea mtoto wake kupata madhara makubwa ya kisaikolojia na kimwili. Kampeni hii ambayo imejikita katika kutoa msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa ukatili na dhuluma, ilichukua hatua mara moja kuhakikisha kwamba haki inatendeka. 

"Nilijua tu kwamba siwezi kukabiliana na hili peke yangu," alisema Asia. "MSLAC walikuwa msaada mkubwa, si tu katika kushughulikia kesi hiyo mahakamani, bali pia katika kutoa ushauri nasaha kwa Aisha ambaye alikuwa amevunjika moyo.

" Asia ana matumaini kuwa haki itatendeka na kwamba matukio kama haya yatapungua kwa kuelimisha jamii juu ya madhara ya ukatili wa kingono na umuhimu wa kulinda watoto wetu. 

"Msaada huu umenipa nguvu mpya," Asia aliongeza. "Ni muhimu sana kwa jamii yetu kujua kwamba kuna sehemu za kupata msaada na kwamba hakuna mtu anayestahili kupitia unyama kama huu peke yake.

" MSLAC inaendelea kusimama imara katika harakati za kumaliza ukatili wa kingono, ikisisitiza umuhimu wa ufikiaji wa haraka na wa haki kwa waathiriwa.