Dawati la Msaada wa Kisheria la Halmashauri ya Jiji la Tanga limekamilisha rasmi ziara yake ya utoaji elimu ya kisheria katika kata zote 27 za jiji hilo. Hatua hii ilihitimishwa jana kwa ziara katika kata za Majengo na Chumbageni, ambazo zilikuwa za mwisho kufikiwa. Katika ziara hiyo, wananchi walipewa elimu kuhusu haki zao za kisheria na huduma zinazotolewa na dawati hilo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote.
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango