Dawati la msaada wa kisheria kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii Mbeya DC limewafikia wananchi wa Kata ya Isuto katika Halmashauri ya Mbeya, likitoa elimu ya kisheria muhimu kwa jamii inayoishi kwa asilimia 89 ya ardhi ya kilimo. Huku msimu wa kilimo ukiwa umeshika kasi, wananchi walipata elimu wakiwa mashambani na katika vikundi vya uzalishaji mali. Huduma zilizotolewa zilihusu:
Huduma ya msaada wa kisheria chini ya MSLAC.
Umuhimu wa kuandika wosia kwa ajili ya kutatua changamoto za urithi.
Haki za ardhi na jinsi ya kuzilinda. Kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia.
Haki za watoto na namna ya kuzuia ukiukwaji wake.
Uzalishaji mali kupitia kilimo bora na chenye tija.
Haki na wajibu ndani ya ndoa.
Umuhimu wa kulinda na kutunza amani ya taifa, kwa kuanzia ngazi ya familia.
Wananchi walionesha shukrani kwa elimu hiyo, wakieleza kuwa itawasaidia sio tu katika kuboresha maisha yao bali pia kudumisha haki, usawa, na amani katika jamii.