Skip to main content

Elimu ya Msaada wa Kisheria Yawafikia Wananchi wa Kijiji cha Mayota, Mbarali – Mbeya

Submitted by admin on 25 February 2025

Mbarali, Mbeya – Wananchi wa Kijiji cha Mayota, Kata ya Legelele, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, wamepata fursa ya kupokea elimu ya msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Samia Legal Aid Campaign (MSLAC), inayolenga kuwawezesha wananchi kuelewa haki na wajibu wao kisheria.  

Elimu hiyo imejikita katika masuala mbalimbali ya sheria, ikiwemo haki za ardhi, mirathi, ndoa, kesi za jinai, unyanyasaji wa kijinsia, na mikataba ya ajira. Wataalamu wa sheria kutoka MSLAC wamewahimiza wananchi kutumia njia mbadala za utatuzi wa migogoro kama usuluhishi na maridhiano ili kuepusha gharama na muda mrefu wa kesi mahakamani.  

Image

Akizungumza katika mafunzo hayo, mmoja wa watoa elimu alisema: *"Ni muhimu kwa wananchi kuelewa haki zao ili waweze kuzitetea na kuepuka migogoro inayoweza kuepukika kwa kuzingatia sheria."*

Wananchi wa Mayota wameipongeza kampeni hii, wakisema kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kufanya maamuzi sahihi na kujilinda dhidi ya manyanyaso ya kisheria.  

MSLAC inaendelea kutoa elimu ya msaada wa kisheria katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni jitihada za kuhakikisha haki inapatikana kwa wote na wananchi wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kisheria yanayowahusu.

#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya