Simanjiro, Tanzania – Wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Orkirung'rung, iliyopo katika Kijiji cha Orkirung'rung, Kata ya Endonyongijape, Wilaya ya Simanjiro, wamepatiwa elimu muhimu kuhusu haki za mtoto na madhara ya ukatili wa kijinsia.
Elimu hii ya msaada wa kisheria ilitolewa kwa lengo la kuwajengea uelewa na kuwawezesha wanafunzi na walimu kutambua haki zao, kujikinga na ukatili wa kijinsia, na kujifunza namna ya kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za watoto.
Katika kampeni hiyo, Afisa wa Dawati la Msaada wa Kisheria aliambatana na watetezi wa haki za binadamu kutoka jamii ya wafugaji, ambao walishiriki kikamilifu katika kutoa mafunzo hayo. Ushiriki wa wanajamii katika kutoa elimu hii umeongeza ushawishi wa ujumbe wa kulinda haki za watoto na kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii ya wafugaji.

Wananchi wa eneo hilo wamepokea mafunzo hayo kwa shukrani kubwa, wakisema kuwa elimu hii itasaidia kupunguza visa vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto. Walimu wa Shule ya Msingi Orkirung'rung pia wameonyesha utayari wa kuhakikisha kwamba elimu hiyo inaendelezwa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uelewa wa haki za binadamu, hususan miongoni mwa watoto na vijana, ili kujenga jamii inayothamini na kulinda haki za kila mmoja.
@ikulu_mawasiliano @ikulu_habari @samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa @DBiteko @sisiniTanzania@airtanzania_atcl @arusha_nationalpark #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya #News