Skip to main content

Haki za Msingi za Wananchi (Ibara ya 13-29)

Submitted by admin on 11 December 2024

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua haki za kila raia kupatiwa usawa mbele ya sheria, haki ya kusikilizwa, na kutokubaguliwa. Kampeni hii inalenga kutekeleza masharti haya kwa kuwapa wananchi uelewa na msaada wa moja kwa moja katika masuala ya kisheria. 

Kutoa Haki kwa Wote 

Kwa mujibu wa Ibara ya 107A na 107B, Katiba inasisitiza umuhimu wa mfumo wa mahakama kutoa haki kwa uwazi, haraka, na bila upendeleo. Kupitia kampeni hii, serikali inalenga kufanikisha azma hii kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kama vile Tanganyika Law Society na vyombo vingine vya msaada wa kisheria. 

Kukuza Ushiriki wa Wananchi 

Katiba pia inasisitiza ushiriki wa wananchi katika maamuzi yanayohusu maisha yao. Kampeni hii inahamasisha wananchi kushiriki kwa uelewa katika masuala ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kupata msaada wa kisheria pale wanapohitaji.