Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, ambayo imezinduliwa rasmi katika Mkoa wa Mara, ni sehemu ya juhudi za serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wote, hususan wale wa kipato cha chini au walioko pembezoni. Kampeni hii inalenga kukuza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kikatiba, za kisheria, na fursa za msaada wa kisheria zinazopatikana. #MSLAC #SSH #sisiNitanzania #matokeoChanya