Skip to main content

HOTUBA YA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA Dkt DAMAN NDUMBARO: MSLAC KAGERA

Submitted by admin on 14 April 2025

Kwa upande wa usimamiwaji wa Haki za Binadamu na Watu, Wizara yangu imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha misingi ya Haki za Binadamu inazingatiwa nchini. Na wote tumekuwa mashuhuda, katika ngazi za Kimataifa na Kikanda, nchi yetu imekuwa ni kinara wa usimamiaji mzuri wa Haki za Binadamu, hivyo ninawasihi Wananchi wa Kagera na Watanzania kwa ujumla tuendelee kuitunza amani na kila mmoja atimize wajibu wake katika kulinda na kutetea haki za kila kundi.

Image

Ni azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendeleza sifa hii njema ya Tanzania kwa kudumisha utawala wa sheria; uzingatiwaji wa haki za binadamu na watu na kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wotehususani kwa makundi maalum na wananchi wasiokuwa na uwezo. Dhamira ya Serikali ni kujenga jamii yenye usawa mbele ya sheria; jamii  ambayo inaheshimu na kuthamini utu wa kila mmoja kuanzia mtoto hadi mzee. Na haya ndiyo maono ya Mhe. Rais katika utekelezaji wa kampeni hii. Jamii inayozingatia haki, usawa, daima huwa na amani. Tunahitaji kuwa na jamii inayoheshimu haki za binadamu.

kupitia Kampeni hii wale wote wanaoathiriwa na vitendo vya ukatili ikiwemo wanawake, watoto, wanaume na makundi mengine  watapata fursa ya kusikilizwa na wale walioathirika na vitendo vya Ukatili wa Kijinsia watasaidiwa waweze kupata haki zao au kuelekezwa mahali sahihi pa kuwasilisha changamoto zao. 

Vilevile, niwaombe wazazi na walezi wote tufuatilie mienendo ya watoto wetu ili kuwakinga na matukio ya ukatili. Jukumu la kuwalinda watoto wetu na jamii kwa ujumla ni letu sote. Tutimize wajibu wetu!!

Lengo letu ni kuhakikisha tunaongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususan haki za wanawake na watoto; 

tunaimarisha huduma ya  ushauri  wa kisheria na unasihi kwa waathirika na manusura wa ukatili wa kijinsia; tunaongeza uelewa kwa wananchi kuhusu  elimu ya sheria kwa umma, masuala ya  haki na wajibu na misingi ya utawala bora, tunaendelea na  utatuzi wa migogoro ya wananchi katika maeneo ya kijamii,  na kuongeza uelewa kwa watendaji katika ngazi za kijamii:  

Dakt. Dammas Ndumaro-Waziri wa katiba na Sheria.

Image