Arusha – Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imeendelea kuwa mwanga wa matumaini kwa wananchi wa Arusha, ambapo mmoja wa wanufaika wake, Raymond Mkini, amepata msaada wa Shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu baada ya kujeruhiwa katika ajali.
Raymond Mkini, mkazi wa Sombetini, Arusha, alikumbwa na mkasa wa kuangukiwa na ukuta wakati akitekeleza majukumu yake, hali iliyosababisha kuvunjika kwa mgongo na hatimaye kupooza. Kwa kipindi cha miaka miwili, alikosa msaada wowote hadi Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ilipoingilia kati na kuhakikisha anapata haki yake.
Kupitia kampeni hii, mawakili walimsaidia Raymond kupata fidia ya Shilingi milioni 15 kwa ajili ya kugharamia matibabu yake nje ya nchi pamoja na mahitaji ya kujikimu kimaisha. Raymond ameonesha shukrani na matumaini kwamba Rais Samia Suluhu Hassan atawezesha safari yake ya matibabu haraka iwezekanavyo ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imeendelea kuwa mkombozi kwa wananchi wengi kwa kutatua migogoro na kutoa msaada wa kisheria, hasa kwa wale wasio na uwezo wa kumudu gharama za kisheria. Hii inaonesha dhamira thabiti ya serikali katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote bila ubaguzi.
Wananchi wengi wamepongeza juhudi hizi, wakisema kuwa kampeni hii ni tumaini jipya kwa wale wanaokumbwa na matatizo ya kisheria na wanahitaji msaada wa haraka na wenye tija. Tukio la Raymond Mkini ni miongoni mwa mifano hai inayoonesha umuhimu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika jamii, ikileta suluhisho la haki kwa wote na kuimarisha maisha ya Watanzania.
#mslac #sisinitanzania #katibanasheria #katibanasheria #ssh #matokeochanya #ccm #hakikwawote #kaziiendelee #habari