Skip to main content

KAMPENI YA UTOAJI WA MSAADA WA KISHERIA KUFIKA MIKOA YOTE NCHINI

Submitted by admin on 10 May 2024

Katıka kuhakikisha upatikanaji wa msaada wa kisheria Nchini Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana, Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ametoa maelekezo kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha kampeni ya utoaji wa msaada wa kisheria ya ‘Mama Samia Lagal Aid’ inawafikia wananchi wa Mikoa yote nchini. Ambapo mpaka sasa tayari kampeni hiyo imefika katika Mikoa 6 na hivi karibuni itafika Mkoani Njombe. 

Waziri Pindi Chana pia ameweka wazi kuwa Rais Dkt. Samia ameiwezesha Wizara yake rasilimali watu pamoja na rasilimali fedha ili kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na Wananchi wengi wanapata msaada wa kisheria bila malipo.