Skip to main content

Katika Hotuba ya kuhitimisha mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu

Submitted by admin on 20 January 2025

Akizungumza na Wananchi kupitia Vyombo vya Habari na nukuu “Katika Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai, Mwakani 2025 tutakamilisha Sera na Kufanya marekebisho ya Sheria mbalimbali zinazohusiana na masuala ya Haki Jinai. Tutaendelea pia kutoa Msaada wa Kisheria kwa wahitaji; hadi sasa jumla ya Wananchi laki nne tisini na tano elfu na mia tano hamsini na mbili, wamekwisha nufaika na Msaada wa Kisheria wa Kampeni ya Mama Samia Legal Aid chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.”

Hotuba ya Mhe. Rais, inaonyesha utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 na utekelezaji wa Sheria ya Utoaji wa Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017 ambapo Serikali inaelekezwa kuhakikisha Huduma za Msaada wa Kisheria inatolewa kwa Wananchi wenye uhitaji. Aidha, inaonesha dhamira ya dhati ya Mhe. Rais, ya kuleta ukombozi kwa wanyonge hususani wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za Mawakili, kupunguza malalamiko ya Wananchi katika sekta ya Sheria na kupunguza mrundikano wa mashauri Mahakamani na katika Vyombo vingine vya Haki.