Skip to main content

Kauli Mbiu ya Kampeni hii ni “Msaada wa Kisheria kwa Haki , Usawa, Amani na Maendeleo”.

Submitted by admin on 14 April 2025

Kauli mbiu hii inaashiria azma ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kulinda, kukuza  na kutetea haki za wananchi wote hususan wanyonge kwa kuhakikisha kwamba kunakuwa na uzingatiaji wa misingi ya utawala bora na kuheshimu utawala wa sheria katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Hakika Kampeni hii inatekeleza falsafa ya 4R ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo ni Maridhiano (Rencoliation), Ustahimilivu (Resiliance), Mageuzi (Reforms), na Kujenga Upya Taifa (Rebuilding) kwani bila misingi imara ya utawala wa sheria na utaoaji haki ambayo ni  majukumu ya muhimu ya  Wizara ya Katiba na Sheria ni vigumu kutekeleza falsafa hii. Dakt. Dammas Ndumbaro- Waziri wa katiba na Sheria