Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kushirikiana na Wizara ya katiba na sheria, inatarajia kuzindua rasmi Kampeni ya Msaada wa Kisheria visiwani Zanzibar tarehe 23 Aprili 2025. Uzinduzi huu utafanyika katika viwanja vya Mkwajuni, Wilaya ya Mjini, Unguja.
Mgeni rasmi katika hafla hii atakuwa Mheshimiwa Dkt. Haroun Ali Suleiman, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
Kampeni hii inalenga kutoa elimu ya kisheria na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wote, hususan wanawake, watoto, na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu. Aidha, inakusudia kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kisheria na kuendeleza utawala wa sheria nchini.
Shughuli zitakazofanyika siku ya uzinduzi ni pamoja na:
Ushauri wa kisheria kwa wananchi.
Semina na warsha za elimu ya sheria.
Wananchi wote wanahimizwa kuhudhuria uzinduzi huu na kushiriki kikamilifu katika kampeni hii ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wote