Maafisa Maendeleo kutoka Dawati la Msaada wa Kisheria katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wametembelea Shule ya Msingi Msasani B na kutoa mafunzo maalum kwa wanafunzi kuhusu ukatili wa kijinsia na njia bora za kujilinda dhidi ya vitendo hivyo.
Katika mafunzo hayo, wanafunzi walielimishwa kuhusu aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia, athari zake kwa wahanga na jamii kwa ujumla, pamoja na hatua za kuchukua ili kujikinga na kuripoti matukio ya ukatili. Mafunzo hayo yalilenga kuongeza uelewa wa watoto kuhusu haki zao na kuwajengea ujasiri wa kupinga ukatili wa aina yoyote katika mazingira yao ya kila siku.
Maafisa hao walisisitiza umuhimu wa kushirikiana na wazazi, walimu, na viongozi wa jamii katika kupambana na ukatili wa kijinsia, huku wakihamasisha wanafunzi kuwa mabalozi wa mabadiliko kwa wenzao.
Hatua hii ni sehemu ya jitihada za serikali na wadau wa haki za binadamu katika kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama na yenye ulinzi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.
#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya