Skip to main content

MAAFISA MAENDELEO DAWATI LA MSAADA WA KISHERIA WATOA ELIMU KWA WANANCHI WA CHITOHOLI JUU, MTWARA

Submitted by admin on 25 February 2025

TANDAHIMBA, MTWARA – Februari 25, 2025   Maafisa Maendeleo kutoka Dawati la Msaada wa Kisheria katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, leo walitoa elimu juu ya msaada wa kisheria wa Mama Samia kwa wakazi wa Kijiji cha Chitoholi Juu, Kata ya Mkundi. 

Katika mkutano huo, wananchi walielimishwa kuhusu haki zao za kisheria na namna ya kupata msaada wa kisheria bila gharama kupitia mpango huu wa serikali. Maafisa waliwasihi wananchi kuwa mabalozi wa elimu hiyo kwa wenzao ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo, ili kuhakikisha taarifa sahihi zinawafikia watu wengi zaidi.  

Msaada wa kisheria wa Mama Samia umekuwa mkombozi kwa wananchi wengi, hasa wale wanaokumbana na changamoto za kisheria lakini hawana uwezo wa kupata huduma za mawakili. Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba inaendelea kusimamia utekelezaji wa mpango huu kwa kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati.  

Wananchi walioshiriki mkutano huo walipongeza juhudi hizo na kuahidi kusambaza elimu waliyoipata kwa jamii zao.  

#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya