Skip to main content

Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Dawati la Huduma za Msaada wa Kisheria wa Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign - MSLAC)

Submitted by admin on 24 December 2024

Image

Wametembelea Kituo cha Masister cha “Moyo Safi” kilichopo Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Kituo hiki kimejikita katika kusaidia wanawake wajane, wanawake waliozalishwa na kutelekezwa, pamoja na wale wenye changamoto za kiuchumi, kwa kuwapatia mafunzo ya ujuzi ili kuwawezesha kujitegemea na kujenga maendeleo yao.

Kituo cha "Moyo Safi" kilianzishwa mwaka 2017 kwa lengo la kutoa elimu ya kujitambua kupitia mpango maalum unaoitwa “Training for Transformation” (Mabadiliko ya Dhati). Kupitia mpango huu, wanawake walipata fursa ya kufanyiwa mafunzo ya kuimarisha uwezo wao wa kujitambua, kutambua vipaji vyao, na kutumia ujuzi walionao kwa manufaa ya maisha yao.

Image

Katika ziara hii ,MSLAC Imewapa elimu ya kina kuhusu mikopo, ajira, na kujiajiri kwa kutumia ujuzi waliopata. Pia, kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake hawa, zikiwemo: 

- Migogoro ya ndoa. 

- Masuala ya ardhi. 

- Mirathi. 

- Madai ya matunzo ya watoto. 

- Kesi za jinai.

Dawati la Msaada wa Kisheria kupitia kampeni ya Mama Samia limekuwa likitoa ushauri na usuluhishi wa migogoro ili kuhakikisha upatikanaji wa haki, usawa, amani, na maendeleo kwa jamii nzima. #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano