Skip to main content

Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wamefanikiwa kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi wa Mtaa wa Kasulu, Kata ya Ilala, wakati wa mashindano ya soka ya KHIMJI ILALA SUPER CUP

Submitted by admin on 4 January 2025

Lengo kuu la elimu hiyo ni kuhakikisha haki za binadamu na makundi yenye uhitaji maalum wa msaada wa kisheria zinalindwa na kutetewa. 

Elimu hiyo ilihusu masuala muhimu kama haki za mirathi, ndoa, ukatili wa kijinsia, matunzo ya watoto, na namna ya kushughulikia migogoro mbalimbali. Kupitia elimu hii, wananchi walihamasishwa kutumia njia mbadala za usuluhishi kama vile upatanishi, maridhiano, na mashauriano ili kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani. #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @IkuluMawasiliano