Skip to main content

Maafisa wa Maendeleo ya Jamii Wilayani Ikungi Watoa Elimu ya Msaada wa Kisheria kwa Wananchi wa Minyughe

Submitted by admin on 28 February 2025

Maafisa wa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, wameendelea na juhudi za kuwapatia wananchi elimu ya msaada wa kisheria, safari hii wakifika katika Kata ya Minyughe.  

Image

Maafisa wa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, wameendelea na juhudi za kuwapatia wananchi elimu ya msaada wa kisheria, safari hii wakifika katika Kata ya Minyughe.  

Maafisa hao wamesisitiza kuwa elimu ya kisheria ni nyenzo muhimu kwa wananchi katika kuhakikisha wanajua namna bora ya kushughulikia matatizo yao kwa mujibu wa sheria, badala ya kutumia njia zisizo rasmi ambazo mara nyingi husababisha migogoro mikubwa zaidi.

Image

Wananchi wa Minyughe wameonyesha kufurahishwa na elimu waliyopewa na kuomba mwendelezo wa kampeni hizi ili kusaidia jamii nzima kuelewa haki na wajibu wao kwa mujibu wa sheria. Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wameahidi kuendelea kutoa elimu hiyo katika vijiji vingine vya wilaya ya Ikungi ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na msaada wa kisheria.

Image

@ikulu_habari @samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa @biteko

@sisinitanzania

@airtanzania_atcl @arusha_nationalpark #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya #news