Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Stephen Mashauri Ndaki akiongoza kikao cha maandalizi ya Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia (MSLAC) mkoani Kagera uzinduzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 Aprili, 2025 katika viwanja vya Jamhuri (Mashujaa) mkoani humo.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria wa Wizara Ester Msambazi pamoja na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ikiwa ni sehemu ya kupeana majukumu na kubadilisha uzoefu ili kufanikisha hafla ya uzinduzi na utekelezaji wa Kampeni mkoani Kagera.