"Nimpongeze Mhe. Rais kwa kuendelea kuboresha Mfumo wa Haki Jinai ikiwemo kuongeza uelewa wa Wananchi kuhusu maendeleo ya Kisheria na kuimarisha upatikanaji Haki kwa wote hususani kwa wale wasiokuwa na uelewa kuhusu masuala ya Kisheria na wale walio na changamoto za Kisheria wanapata Haki kupitia Huduma za Msaada wa Kisheria.
Upendo wa Mheshimiwa Rais kwa Wananchi, ndio umepelekea yeye kuridhia changamoto zao za masuala ya Kisheria na hatimaye kupatikana kwa Kampeni hii ambayo imekua mkombozi mkubwa kwa Wananchi" DKT.Damas Ndumbalo Waziri wa Katiba na Sheria