Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) imeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria zinafikia Watanzania kwa ufanisi. Katika hatua ya kuimarisha utekelezaji wa kampeni hii, mafunzo maalum yametolewa kwa waratibu wa MSLAC kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mafunzo haya yamewalenga waratibu wa kampeni kwa lengo la kuwaongezea ujuzi na maarifa ya jinsi ya kusimamia, kuratibu, na kufikisha huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kwa ufanisi zaidi.