Katika video hii, Mhe. Agness Kaiza, Mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora, Katiba na Sheria, anatoa salamu maalum wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia uliofanyika mkoani Tanga tarehe 08 Machi 2025.
Mhe. Kaiza amesisitiza umuhimu wa wananchi kufahamu haki zao na kutumia huduma ya msaada wa kisheria kama nyenzo ya kuondoa dhuluma, migogoro na ukatili wa kijinsia katika jamii. Amepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote bila ubaguzi.
⚖️ Huduma zinazotolewa kupitia kampeni hii ni pamoja na:
Elimu ya haki za binadamu na sheria
Ushauri na msaada wa kisheria kwa migogoro ya ardhi, ndoa, familia, na mirathi
Kuzuia ukatili wa kijinsia na dhuluma za majumbani
Njia mbadala za utatuzi wa migogoro (upatanishi na usuluhishi)
📍 Tazama video hii upate ujumbe mzito kutoka kwa Mhe. Agness Kaiza kuhusu dhamira ya Bunge na Serikali katika kusogeza haki kwa wananchi wote.
🔔 Subscribe kwenye channel yetu kwa taarifa na elimu zaidi kuhusu sheria na haki.
#MamaSamia #AgnessKaiza #MsaadaWaKisheria #UzinduziTanga #MoCLA #KatibaNaSheria