Skip to main content

MIGOGORO YA ARDHI KERO SUGU IRAMBA

Submitted by admin on 11 January 2024

MIGOGORO ya ardhi imetajwa kuwa ni ndio moja ya kero kubwa kwa wananchi wilayani Iramba Mkoani hapa na imesababisha kutumia muda mwingi kutafuta haki hiyo maeneo mbalimbali ya utoaji haki.

Hayo yalibainishwa wakati wa mkutano wa hadhara kati ya wananchi na timu ya kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia uliofanyika Kata ya Shelui Wilaya ya Irimba Mkoani Singida.

Kero hiyo ya migogoro ya ardhi imetajwa kuwa ni kubwa kwa wananchi hao na imesaababisha kutumia muda mwingi kuitafuta haki hiyo kwenye maeneo ya utoaji haki. Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo Johashi Shimikila akizungumza kwenye mkutano huo alisema kero hiyo inaongoza kati ya kero nyingi walizonazo wananchi wa wilaya hiyo.

Shimikila alisema wanashuru wajumbe wa kampeni hiyo kufika hapo na kilio chao namba moja ni kero ya ardhi ambayo imesabaisha kupoteza mud na fedha kiitafuta. Kadhalika alisema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujna na kampeni hiyo ambayo inatoa fursa kwa wananchi kusikilizwa na kusaidiwa kupata haki zao.

“Binafsi nimetoa kero yangu hii ambayo imekuwa ikinisumbua mimi na wananchi wenzangu ya migogoro ya ardhi hivyo kupitia kampeni hii nimepata Imani ya kuhudumiwa “alisema.

Aliitaja aina ya migogori iliyopo kuwa ni kugombea mipaka ya mashamba na wengine kudhulimiwa ardhi kutokana na kushindwa kuwalipa mawakili wa kuwasaidia kesi zao.

Aliongeza migogoro mingine ni kucheleweshwa kwa hati za maeneo yao waliopimiwa jambo ambalo linawachelewesha kuendeleza maeneo yao . Mkazi mwingine Sada Salula alisema wanawake wengi waliofiwa na waume wao hasa maeneo ya Vijijini wamekuwa wakinyang’anywa ardhi kwa madai kuwa hawana haki ya kumiliki.

Sada alisema wajane hao wamekuwa wakifukuzwa kwenye familia waliyokuwa wakiishai na wenzao wa kwa madai kuwa mila haziruhusu mjane kumiliki ardhi.

“Mimi hapa ni miongoni mwa wajane niliyenyang’anywa ardhi baada ya mume wangu kufa kwa sa nahangaika na watoto wangu nimeshafukuzwa nimeona nifike hapa kutoa kilio change kwenye kampeni hii ya Mama Samia”aliangua kilio. Mkuu wa Wilaya ya Iramba ,Suleiman Mwenda alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo ya ardhi na kuwataka wananchi kufika kwenye kampeni hiyo ili kupata haki yao.

“Kwa kweli katika malalamiko mengi yanayokuja ofisini kwangu kama Mkuu wa Wilaya ni masuala ya ardhi,ardhi imekuwa tatizo sana katika wilaya yetu ya Iramba ,kesi ni nyingi mno kutokana na uhaba wa watoa huduma za kisheria kumeibuka na wanasheria feki wanaowatapeli wananchi”, alisema.

Mwenda alisema anaamini kupitia kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria mama Samia itawasaidia wananchi wengi kupata haki zao kwa sababu inawataalamu wa kila idara na aliwataka wananchi ahao kujitokeza mbele ya timu hiyo ili kusikiliza na kutatuliwa kero zao zinazowakabili.

Kiongozi wa kampeni ya huduma ya msaadw wa kisheria ya mama Samia Wilaya ya Iramba ,Godfrey Ngangaji alisema kampeni hiyo ilizinduliwa Aprili 2023 na inaendelea kuzinduliwa kila Mkoa mpaka sasa imefika Mikoa sita.

Ngangaji alisema lengo la kampeni hiyo ni kuwasaidia wananchi kupata haki zao na imekuwa ikifanyakazi na watu wa idara zinazotoa haki ambazo ni mahakama,wanasheria,jeshila Polisi,Maofisa maendeleo ya jamii,Ustawi wa jamii ,Ofisi ya Mwendesha mashtaka na watalamu wengine wa sheria.