Skip to main content

Mkutano wa Hadhara Kijijini Roondoo Watoa Elimu ya Msaada wa Kisheria kwa Wananchi

Submitted by admin on 12 February 2025

Image

Katika jitihada za kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kisheria, mkutano wa hadhara umefanyika katika Kijiji cha Roondoo, Kata ya Romu, ambapo wananchi walipata fursa ya kupokea elimu kuhusu huduma ya msaada wa kisheria.

Wananchi walionyesha furaha na shukrani kwa elimu waliyopewa, wakisisitiza umuhimu wa elimu hiyo kuwa endelevu ili kuendelea kuwasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili.

Image

Mkutano huu ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuhakikisha wananchi wanapata uelewa mpana wa haki zao na namna ya kuzitetea kupitia taratibu za kisheria.

#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya