Mkoa wa Kigoma umeendelea kunufaika na huduma za msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Samia Legal Aid Campaign (MSLAC), ambayo inalenga kutoa elimu ya kisheria na kuhakikisha haki za wananchi zinazingatiwa. Msaada huu wa kisheria unalenga makundi mbalimbali ya jamii, yakiwemo wakulima, wavuvi, wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu ambao mara nyingi wanakabiliwa na changamoto za kisheria kutokana na ukosefu wa elimu na rasilimali.