Skip to main content

MSLAC ILIVYOMGUSA MAMA ADAMU

Submitted by admin on 21 December 2024

Mama Adamu, mkazi wa Mtaa wa National, Kata ya Manyoni, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, mkoa wa Singida, amekuwa akikabiliwa na changamoto kubwa za maisha baada ya kutelekezwa na mume wake kwa muda mrefu sasa. Pamoja na changamoto hizo, mama huyu alipata kimbilio katika Idara ya Maendeleo ya Jamii. 

Kupitia jitihada za watumishi wa ofisi hiyo, walifanikiwa kuchanga kiasi cha shilingi 110,000, ambacho kilitumiwa kumnunulia bidhaa za biashara, ikiwemo nyanya, vitunguu, dagaa, nyanya chungu, na gunia moja la mkaa. Bidhaa hizo zitamwezesha kuendesha biashara yake katika kibanda alichonacho tayari. 

Mama Adamu ameonyesha furaha na shukrani zake kwa msaada huo, akisema utamsaidia sana katika kujenga maisha mapya na kulea watoto wake wawili. Idara ya Maendeleo ya Jamii imeahidi kuendelea kushirikiana naye na watu wengine wenye changamoto kama hizi ili kuboresha maisha yao.