Skip to main content

MSLAC, KUHAKIKISHA HAKI ZA KISHERIA KWA WATANZANIA WOTE

Submitted by admin on 27 December 2024

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia 

( MSLAC) inalenga kutoa msaada wa kisheria kwa Watanzania wote, hususan wale wanaokumbwa na changamoto za kupata huduma za kisheria kwa sababu ya ukosefu wa fedha au uelewa. Kampeni inatoa msaada katika nyanja mbalimbali za sheria ikiwemo haki za familia, ardhi, ajira, na haki za raia. 

MSLAC imeleta manufaa makubwa kwa Watanzania kwa kuwawezesha kupata msaada wa kisheria bila gharama kubwa, na kuwasaidia watu wengi kutatua migogoro yao kwa njia ya kisheria. Kampeni hii pia inatoa fursa kwa wananchi kupata elimu ya kisheria, ambayo inawasaidia kutambua haki zao na jinsi ya kuzitetea. Watanzania wanahamasishwa kujitokeza kwa wingi na kutumia huduma hizi muhimu ili kuhakikisha haki zao zinatetea na kuheshimiwa.