Skip to main content

#MSLAC KUTATUA MGOGORO ULIODUMU KWA ZAIDI YA MIAKA 5 BAINA YA NDUGU WAWILI.

Submitted by admin on 31 May 2024

Judith Komba Mkazi wa Kijiji cha Ibumi akitoa shukrani kwa Mhe. Rais Doct. Samia Suluhu Hassan kwa huduma ya Msaada wa Kisheria iliyowafikia katika kijiji cha Ibumi baada ya timu ya wataalam kutatua mgogoro ulidumu takribani miaka 5 kati yake na mdogo wa Melina Komba ambaye ni mjumbe wa Serikali ya Kijiji. Judith aliamua kujenga nyumba ya kuishi katika eneo la familia hali iliyosababisha kuibuka kwa mgogoro kati yake na familia yake na kupelekea Judith kuondoka na kwenda kuishi Songea ndipo Melina akachukua matofali 700 ya Judith. Judith alipoamua kurudi kuishi Ibumi akakuta matofali hayapo ndipo mgogoro kati yao ukaanza. Melina amehaidi kurudisha matofali 1000 badala ya 700 ndani ya muda wa wiki moja na ndugu hawa wamepatana na wamekubaliana kuishi kwa amani. 

@samia_suluhu_hassan @katibanasheria_ @ikulu_mawasiliano @kassim_m_majaliwa @hakingowinews @pindi.chana @msambaziester @katibanasheria_ @katibayawatu #MSLAC #Katibanasheria #Ikulu #KaziIendelee #SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu #SSH #KaziIendelee #Nchiyangukwanza