Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imezinduliwa rasmi leo, tarehe 24 Januari 2025, katika Uwanja wa Mwanga Community Center, mkoani Kigoma. Uzinduzi huu umehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, pamoja na viongozi wengine wa serikali na wadau mbalimbali.
Kampeni hii inalenga kutoa huduma za kisheria bure kwa wananchi wa Kigoma, ikijikita katika maeneo muhimu kama msaada wa kisheria kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi, na masuala mengine ya kisheria. Huduma hizi zitatolewa kwa muda wa siku tisa katika halmashauri tisa za mkoa wa Kigoma, ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati na kwa njia ya amani.
Kwa mujibu wa Waziri Ndumbaro, kampeni hii itasaidia kutatua migogoro mbalimbali kupitia njia za amani, usuluhishi, mahakama, kiutawala, na kwa njia za kiuchunguzi. Aidha, amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika kampeni hii ili kufaidika na huduma zinazotolewa.
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango @biteko
@katibanasheria_ @profkabudipjam @Victoria
.mwanziva @tanganyikalawsociety @boniface_a_k_mwabukusi