Skip to main content

MSLAC MKOMBOZI

Submitted by admin on 18 March 2025

Timu iliohusika kwenye kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama samia wilaya ya  Hai, imemkabidhi Mzee Assery Mushi, Shamba lake lenye ukubwa wa heka 1,  katika kitongoji cha Landi, kijiji cha Kikavu chini, kata ya weruweru, wilaya ya Hai, Mkoa wa kilimanjaro, kutokana na Mgogoro wa shamba hilo kudumu kwa muda mrefu kati yake na Bw. Jacob Ogalo, hivyo baada ya timu hiyo kusikiliza  pande zote mbili, pamoja na kujilizisha kupitia Maamuzi/ hukumu  iliyotolewa na baraza la Aridhi la wilaya, Mzee Assery Mushi amekabidhiwa rasmi shamba lake na timu hiyo mbele ya uongozi wa kitongoji, kijiji, kata pamoja na majirani katika shamba hilo.

#kazinaututunasongambele #sisinitanzania #matokeochanya #katibanasheria #nchiyangukwanza #kaziiendelee #SSH #MSLAC