Kibaha, 25 Februari 2025 – Timu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) imewasili katika Halmashauri ya Kibaha Mji na kuripoti rasmi katika Ofisi ya Mkurugenzi kwa lengo la kujitambulisha na kuwasilisha ratiba ya utekelezaji wa kampeni hiyo kabla ya kuanza ziara za kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria katika kata mbalimbali.
Baada ya kujitambulisha, timu hiyo imeanza rasmi utekelezaji wa kampeni kwa kutembelea Kata ya Tumbi, ambako imekutana na wananchi ili kusikiliza na kushughulikia changamoto zao za kisheria. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki zao kwa wakati kupitia ushauri wa kisheria, elimu kuhusu sheria mbalimbali, na mbinu za utatuzi wa migogoro kwa njia ya maridhiano.
Kampeni hii ni sehemu ya juhudi za serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi, hususan kwa makundi yenye uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria. MSLAC inaendelea na ziara zake katika kata nyingine ndani ya Halmashauri ya Kibaha Mji kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi zaidi.
#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya