Skip to main content

MSLAC YABADILI MAISHA YA HALIMA, USHINDI DHIDI YA DHULUMA YA MIRATHI.

Submitted by admin on 6 January 2025

Halima, mjane wa miaka 45 kutoka Lyabukande, Shinyanga, alikumbana na changamoto baada ya kifo cha mume wake, Hamisi, pale ndugu wa mume walipotaka kumvua mali zote za familia. Bila uelewa wa sheria, alihisi hana msaada hadi alipopewa msaada na mawakili wa MSLAC.  

Mawakili walimsaidia kisheria, wakaratibu upatanisho uliosababisha kugawanywa haki kwa mali hizo. Halima alipata nyumba, ekari tano za shamba, na mifugo kwa watoto wake. Pia alifundishwa kuandaa wosia na kusimamia mali zake.

Leo, Halima anaishi kwa amani na familia yake na anawahamasisha wanawake wengine kujua haki zao kupitia kampeni ya MSLAC. Kisa chake kinaonesha jinsi msaada wa kisheria unavyoweza kubadilisha maisha.