Mkuranga, Pwani – Mpango wa Msaada wa Kisheria wa Samia (MSLAC) umeendelea kuwafikia wananchi kwa kutoa elimu ya msaada wa kisheria, ambapo safari hii wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Mwandege, iliyopo katika Kijiji cha Mwandege, Kata ya Mwandege, Halmashauri ya Mkuranga, wamepata mafunzo muhimu kuhusu haki za watoto na kupinga ukatili wa kijinsia.
Wakizungumza baada ya mafunzo hayo, baadhi ya walimu walieleza kuwa elimu hii imekuja wakati muafaka kwani itawezesha wanafunzi kuelewa haki zao na kujilinda dhidi ya ukatili wa aina yoyote. Pia, walimu walihimizwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa mwongozo na msaada kwa wanafunzi wanaokumbana na changamoto za kijinsia na kisheria.
MSLAC inaendelea na jitihada zake za kusambaza elimu ya msaada wa kisheria kwa jamii mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya azma ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha haki zinapatikana kwa wote, hususan watoto na makundi maalum. @ikulu_habari @samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa @sisinitanzania
@airtanzania_atcl @arusha_nationalpark #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya #news Image