Skip to main content

MSLAC Yatoa Elimu ya Msaada wa Kisheria kwa Wananchi wa Kijiji cha Kisangile, Kisarawe

Submitted by admin on 28 February 2025

Kisarawe, 28 Februari 2025 – Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) inaendelea kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi wa vijijini, ambapo hivi karibuni imefika katika Kijiji cha Kisangile, Kata ya Masaki, wilayani Kisarawe. 

Image

Katika uhamasishaji huu, wananchi wamepata fursa ya kujifunza kuhusu haki zao za kisheria katika masuala mbalimbali, ikiwemo ardhi, mirathi, ndoa, kesi za jinai, ajira, na unyanyasaji wa kijinsia. Timu ya MSLAC imewahimiza wananchi kuandika wosia na kutumia njia mbadala za utatuzi wa migogoro kama usuluhishi, maridhiano, na majadiliano ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima inayoweza kuathiri maendeleo yao.

Aidha, wananchi wamehimizwa kutumia huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa bure kupitia kampeni hii ili kupata mwongozo sahihi wa kisheria. Kampeni hii inaendelea kuhakikisha kwamba wananchi wa maeneo mbalimbali wanapata uelewa wa kutosha kuhusu haki zao na njia bora za kuzitetea kwa mujibu wa sheria.  
 

Image

Kampeni ya MSLAC itaendelea na ziara zake katika maeneo mbalimbali nchini, ikizingatia dhamira yake ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki bila vikwazo vya kisheria. @ikulu_habari @samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa @sisinitanzania

@airtanzania_atcl @arusha_nationalpark #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya #news Image