Skip to main content

MSLAC Yatoa Huduma za Kisheria Bure kwa Wananchi wa Bukoba Mjini

Submitted by admin on 14 April 2025

Baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) katika Mkoa wa Kagera, huduma za msaada wa kisheria zimeanza kutolewa kwa wananchi katika Viwanja vya Uhuru, katikati ya Bukoba Mjini. Kampeni hii inalenga kuwafikia wananchi wanaokosa fursa za msaada wa kisheria kutokana na changamoto mbalimbali za kiuchumi na kijamii. 

Image

Huduma Zinazotolewa:

•Ushauri wa kisheria kwa masuala ya kifamilia, ardhi, mirathi, ndoa, na haki za binadamu. 

Image

•Usuluhishi wa migogoro ya kijamii na kifamilia. 

•Elimu ya kisheria kwa jamii ili kuongeza uelewa wa haki na wajibu wao.

Image

Mkurugenzi wa MSLAC, Bi. Ester Msambazi, ametoa wito kwa wananchi wote wa Bukoba na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kufaidika na huduma hizi za bure. Alisisitiza kuwa kampeni hii inalenga kuhakikisha haki za msingi za kila Mtanzania zinalindwa na kuheshimiwa, bila kujali hali ya kiuchumi au kijamii ya mtu. 

Huduma hizi zitaendelea kutolewa kwa siku kumi mfululizo, na zinatarajiwa kuwafikia wananchi wengi zaidi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kampeni hii na huduma zinazotolewa, tembelea tovuti rasmi ya MSLAC: http://mslac.or.tz.