Kupitia kampeni hii, masuala yanayohusu migogoro ya ardhi, ambayo mara nyingi huathiri wanawake na makundi mengine yaliyoko pembezoni mwa jamii, yanashughulikiwa kwa ufanisi zaidi. Vilevile, kampeni inatoa elimu ya kisheria kwa wananchi ili waweze kuelewa haki zao na taratibu za kisheria zinazohusika.