Skip to main content

MSLAC Yawafikia Wananchi wa Kijiji cha Tamasenga, Rukwa

Submitted by admin on 28 February 2025

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) imeendelea kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo safari hii imetua katika Kijiji cha Tamasenga, Kata ya Pito, Halmashauri ya Manispaa, mkoani Rukwa.  

Image

Kupitia mnada wa Tamasenga, timu ya MSLAC ilikutana na wananchi wa eneo hilo na kuwapatia elimu ya kisheria kuhusu haki zao, taratibu za kisheria, na namna bora ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili. Elimu hiyo ilihusu masuala ya ardhi, mirathi, ndoa, haki za wafanyakazi, na mbinu za utatuzi wa migogoro kwa njia za amani na maridhiano.

Wananchi wa Tamasenga walielezea kufurahishwa na msaada huo wa kisheria, wakisema kuwa kampeni hii ni muhimu sana kwao, hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili katika kutafuta haki zao.

Image

Wananchi wa Tamasenga walielezea kufurahishwa na msaada huo wa kisheria, wakisema kuwa kampeni hii ni muhimu sana kwao, hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili katika kutafuta haki zao.

Image

Timu ya MSLAC imeahidi kuendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi katika mkoa wa Rukwa na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata fursa ya kujua haki zake na jinsi ya kuzitetea kwa mujibu wa sheria. @ikulu_habari @samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa @biteko

@sisinitanzania

@airtanzania_atcl @arusha_nationalpark #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya #news