Katika juhudi za kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki yake bila vikwazo vya kifedha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelipa gharama zote za huduma za msaada wa kisheria ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo bure kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign - MSLAC).
Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA, Paul Makonda, amepongeza jitihada za Rais Samia katika kuwezesha upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za uendeshaji wa mashauri na huduma za kisheria.
"Kupitia uongozi wake mahiri, Rais Samia amehakikisha kila mwananchi anapata msaada wa kisheria bila malipo yoyote. Kampeni ya MSLAC ni mfano wa uongozi wake wenye kujali wananchi, hasa wale wa kipato cha chini wanaohitaji msaada wa kisheria katika masuala ya ardhi, mirathi, ndoa, makosa ya jinai, ukatili wa kijinsia na ajira," alisema RC Makonda.
Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) imekuwa ikitekelezwa kwa nguvu nchini kote, ikiwahamasisha wananchi kushiriki na kufahamu haki zao za kisheria, huku wakipewa ushauri na msaada wa kisheria kutoka kwa wataalamu wa sheria bila gharama yoyote.
Kwa hatua hii, Rais Samia ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kuimarisha mfumo wa haki kwa wote, kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za msaada wa kisheria, na kuhamasisha utatuzi wa migogoro kwa njia ya maridhiano, usuluhishi na mashauriano.
#mslac #sisinitanzania #katibanasheria #ssh #kaziiendelee #matokeochanya #nchiyangukwanza #hakikwawote