Skip to main content

TANZANIA SIO NCHI MASIKINI

Submitted by admin on 22 November 2024

Kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Tanzania kuwa nchi tajiri yenye rasilimali nyingi lakini yenye changamoto za kuzitumia kwa manufaa ya wananchi inaendana moja kwa moja na mwelekeo wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inatoa mwongozo kuhusu namna rasilimali za taifa zinavyopaswa kutumiwa kwa manufaa ya wananchi wote. Mwelekeo wa Katiba Kuhusu Rasilimali na Ustawi wa Taifa Katiba ya Tanzania ina vipengele mbalimbali vinavyoainisha misingi ya usimamizi na matumizi ya rasilimali za taifa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. 

#katibanasheria #mslac #sisinitanzania@ikulumawasliano@SuluhuSamia@Sheria_Katiba@TanganyikaLaw@matokeochanya