Skip to main content

TLS YAFICHUA CHANZO KIKUU CHA MIGOGORO YA ARDHI MOROGORO

Submitted by admin on 6 January 2026

Mchango wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) umeendelea kudhihirika kwa kiwango kikubwa katika kupunguza migogoro ya ardhi mkoani Morogoro, migogoro ambayo imeendelea kuwa changamoto kubwa kwa wananchi wengi.

Akizungumza katika kliniki ya msaada wa kisheria, Wakili wa Kujitegemea na Wakili Mwandamizi, Hassan Nchimbi, amesema kuwa migogoro ya ardhi ndiyo inaongoza kwa wingi mkoani Morogoro, hali inayosababisha athari za kijamii, kiuchumi na kisheria kwa wananchi.

Wakili Nchimbi amesisitiza kuwa suluhisho la kudumu ni:

Kuwapatia wananchi elimu ya sheria za ardhi

Kufuata taratibu halali za umiliki wa ardhi

Kuepuka mikataba isiyo rasmi

Kutumia vyombo vya kisheria kabla migogoro haijawa mikubwa

Video hii inaeleza kwa kina njia za kuepuka migogoro ya ardhi na umuhimu wa ushiriki wa TLS katika kujenga jamii yenye uelewa wa haki na sheria.

📌 Tazama video hii hadi mwisho upate elimu muhimu ya kisheria.

📌 Usisahau Subscribe, Like, Share na Comment.

#TLS #MigogoroYaArdhi #Morogoro #HassanNchimbi #WakiliMwandamizi #ElimuYaSheria #SheriaZaArdhi #HakiZaArdhi #MsaadaWaKisheria #LegalAidTanzania #HakiKwaWananchi #UtawalaBora #JusticeForAll #AccessToJustice #Tanzania #WananchiKwanza