Skip to main content

TOLEO LA PILI LA UREKEBU WA SHERIA KUU ZA NCHI LA MWAKA 2023 KUANZA KUTUMIKA JULAI MOSI, 2025

Submitted by admin on 30 April 2025

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amelieleza Bunge la Tanzania kuwa Wizara hiyo kupitia kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali imeendelea kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinaenda na wakati na zinaakisi sera na vipaumbele vya serikali katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kuitamaduni, mazingira na kiteknolojia.

Katika kutekeleza hilo, Waziri Ndumbaro aliyekuwa akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na sheria kwa mwaka 2025/26 ameeleza kuwa Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali iliandaa miswada ya sheria 16 pamoja na kuhakiki na kupitisha sheria ndogo 903, kulinganisha na sheria ndogo 885 zilizopitishwa katika kipindi cha Julai- Aprili mwaka 2023/24.

Waziri Ndumbaro katika maelezo yake ameeleza kuwa Wizara yake pia imekamilisha urekebu wa sheria kuu 446 na kuandaa toleo la nchi la sheria zilizofanyiwa urekebu la mwaka 2023, likiwa ni toleo la pili tangu kupatikana kwa uhuru, toleo la kwanza likiwa la mwaka 2002, lililokuwa limefadhiliwa na Benki ya dunia na Toleo hili la pili limeandaliwa kwa fedha za ndani na wataalamu wa ndani, likitarajiwa kuanza kutumika rasmi Julai Mosi 2025 mara baada ya kuzinduliwa na Rais Samia mnamo Aprili, 23, 2025.