Skip to main content

TUWAFIKIE WALIOKIMYA KWA HAKI – BI. ESTHER MSAMBAZI

Submitted by admin on 13 April 2025

Mkurugenzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, Bi. Esther Msambazi, akizungumza katika ufunguzi rasmi wa mafunzo ya utoaji wa msaada wa kisheria mkoani Kagera. Mafunzo haya yamekusudiwa kuwajengea uwezo watoa huduma za msaada wa kisheria, ili waweze kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi, hasa wanawake, watoto, na watu wenye uhitaji maalum.

Kupitia kampeni hii, serikali inalenga kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wote kwa njia ya elimu sahihi na huduma rafiki, zinazoeleweka na kufikika kirahisi kwa wananchi wa kawaida.

🎯 Lengo: Haki kwa wote – si kwa wachache pekee!

📍 Mkoa: Kagera

💡 Kampeni: Mama Samia Legal Aid Campaign

Tazama video hii ujue jinsi kampeni hii inavyowabadilisha watu na jamii kwa ujumla.

🔔 Subscribe, like, na share kufikisha ujumbe huu kwa kila Mtanzania.

#esthermsambazi #kampeniyamamasamia #msaadawakisheria #hakikuwote #kagera #wanawake #watoto #ulemavu #elimuyasheria