Iringa, 7 Februari 2025 — Manispaa ya Iringa imeendelea kutoa huduma muhimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi, hususan katika kutatua migogoro ya ardhi ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa familia na jamii katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.
Huduma hii, inayoratibiwa na maafisa wa sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii, inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki kwa wakati na kwa njia za amani kupitia utatuzi wa kisheria unaozingatia sheria za ardhi na haki za binadamu.
Akizungumza wakati wa utoaji wa huduma hizo, Afisa Dawati la Msaada wa Kisheria wa Manispaa ya Iringa alisema, “Migogoro ya ardhi imekuwa moja ya changamoto zinazoathiri maendeleo ya jamii. Kupitia msaada huu wa kisheria, tunasaidia pande zinazogombana kufikia suluhu ya kudumu kwa njia za kisheria na maelewano.”
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango
@katibanasheria_ @profkabudipjam
.mwanziva @tanganyikalawsociety @boniface_a_k_mwabukusi