Skip to main content

UTOAJI WA MIKOPO NA MASHINE ZA UCHAKATAJI TANGAWIZI KWA WAJASIRIAMALI KIGOMA

Submitted by admin on 25 February 2025

Katika juhudi za kuwawezesha kiuchumi wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, hafla ya utoaji wa mikopo pamoja na kukabidhi mashine za uchakataji wa tangawizi kwa vikundi vya wajasiriamali ilifanyika mkoani Kigoma, katika Kata ya Buhigwe DC, Wilaya ya Buhigwe.

Image

Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi wa serikali, wawakilishi wa vikundi vya wajasiriamali, pamoja na wanufaika wa mpango huo. Akizungumza wakati wa tukio hilo, kiongozi wa hafla hiyo alisisitiza umuhimu wa mikopo na vifaa hivi katika kuinua uchumi wa wanavikundi, kuongeza thamani ya mazao, na kuleta maendeleo endelevu katika jamii.  

Mashine zilizotolewa zitasaidia kuongeza ufanisi katika uchakataji wa tangawizi, kuongeza uzalishaji na kuboresha ubora wa bidhaa zinazotokana na zao hilo, hivyo kufungua fursa zaidi za soko kwa wajasiriamali wa Buhigwe.  

Image

Wanufaika wa mpango huu walipongeza juhudi hizi, wakisema kuwa mikopo na vifaa walivyopokea vitawawezesha kukuza biashara zao na kuinua hali zao za maisha. Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na vikundi vya wajasiriamali ili kuhakikisha kuwa fursa hizi zinawanufaisha walengwa na kuleta maendeleo kwa jamii kwa ujumla.  

#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya