Skip to main content

UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA KASKAZINI UNGUJA – APRILI 2025

Submitted by admin on 23 April 2025

Uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) umefanyika tarehe 23 Aprili 2025 katika Kaskazini Unguja, ukiandaliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora chini ya Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria.

Mgeni rasmi wa tukio hili alikuwa Mhe. Dkt. Haroun Suleiman, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

Kampeni hii inalenga kuhakikisha wananchi wote, hasa makundi maalum kama wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu, wanapata msaada wa kisheria unaoeleweka, kufikika, na wenye tija katika kutatua changamoto zao za kisheria.

Tazama video hii kuona mapokezi, matukio ya uzinduzi na ujumbe muhimu kuhusu haki kwa wote.

#MamaSamiaLegalAid #MSLAC #UzinduziKaskaziniUnguja #Zanzibar #MsaadaWaKisheria #HakiKwaWote #HarounSuleiman #SerikaliYaMapinduzi