Skip to main content

VYETI SASA KUPATIKANA NDANI YA MASAA 48 - MHE WAZIRI JUMA Z. HOMERA , WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA

Submitted by admin on 6 January 2026

Vyeti sasa vinapatikana ndani ya masaa 48 kupitia programu maalumu iliyoanzishwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA). Hatua hii inalenga kuboresha huduma kwa wananchi kwa kurahisisha upatikanaji wa vyeti muhimu kwa haraka na kwa njia ya kidijitali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria, Juma Homera, amesema mfumo huu mpya utapunguza usumbufu, kuokoa muda na kuongeza uwazi katika utoaji wa huduma za usajili nchini.   

#RITA #VyetiNdaniYaMasaa48 #HudumaKidijitali #JumaHomera #KatibaNaSheria